Macho na masikio yote Jumamosi ya leo yataelekezwa Lagos ambako tuzo za AMVCA (Africa Magic Viewr's Choice Awards) zitafanyika. Tuzo za AMVCA zilianzishwa ili kutambua na kusherehekea mchango wa wandaaji filamu, waigizaji na wataalam wa Afrika kufuatia mafanikio ya Bara hili katika tasnia ya filamu na televisheni.
Tanzania inajivunia kuwa sehemu ya mashuhuda, kufuatia kupendekezwa katika vipengele kadhaa kutoka tamthilia maarufu, Siri ya Mtungi iliyoingia katika vipengele vifuatavyo:
· Best Make Up – Rehema Samo
· Best Wardrobe – Doreen Estazia Noni
· Best Art Direction – Kyle Quint
· Best Sound Editor – Jordan Riber
· Best Actor in a Drama – Juma Rajab
· Best Indigenous language movie/series – Jordan Riber
· Best TV Series (comedy/drama) – John Riber
Timu nzima itakayoondoka itasindikizwa na Waziri wa Habari, Dr. Fenella Mukangara.
Tuzo za mwaka jana zilihudhuriwa na baadhi ya majina makubwa katika uigizaji barani Afrika. Baadhi ya filamu ambazo zilibeba tuzo zilikuwa Otelo Burning (Filamu bora), Skeem (Filamu bora - Ucheshi) na The Mirror Boy (Filamu Bora ya tamthlia). Waigizaji Bora wa kike na kiume walikuwa OC Ukeje toka Nigeria na Jackie Appiah wa Ghana.
Watazamaji wanaweza kuangalia tukio zima la utoaji wa tuzo kupitia Africa Magic kuanzia saa moja jioni.
Tunaitakia Siri ya Mtungi kila la heri.